Yanga
na KCCA zitapambana Juni 6 jijini Mwanza katika mechi maalum ya kirafiki kujiandaa na
msimu mpya.
Washambuliaji
hao, Tony Odur, Herman Wasswa, Gaddafi Kiwanuka na Brian Majwega ndiyo walikuwa
tishio kubwa kwa mabaki msimu uliopita katika Ligi Kuu ya Uganda na mwisho
waliiwezesha timu yao kubeba ubingwa.
Kikosi
cha Ernies Brandts ndicho kilimaliza ligi msimu uliopita kikiwa na mabeki
wagumu zaidi kupitika hadi mwisho wa ligi wakaisaidia timu yao kubeba ubingwa.
Maana
yake mechi hiyo itakuwa ni ya ushindani mkubwa kutokana na sifa hizo mbili za
timu hizo ambao ndiyo mabingwa wa Tanzania Bara na Uganda.
Yanga
itacheza mechi mbili dhidi ya KCCA katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
na baadaye kwenye Uwanja wa Kambarage katika Manispaa ya Shinyanga mjini.
na
timu hizo
awali
Yanga walipanga kuweka kambi nchini Uholanzi lakini wakaahirisha kwenda
kutokana na kutakiwa kushiriki michuano ya Kagame ambayo hata hivyo walijitoa
baadaye.
0 COMMENTS:
Post a Comment