June 27, 2013


Bony akishangilia baada ya kuifunga Stars bao la nne..


Klabu ya Swansea City iko katika hatua za mwisho kumsajili mshambuliaji Wilfried Bony wa Vitesse Arnhem kuziba pengo la Michu.

Swansea iko tayari kutoa kitita cha pauni milioni 10.2 kumnasa mshambuliaji huyo raia wa Ivory Coast aliyefunga bao la nne wakati timu yake ilipoivaa Taifa Stars kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuibuka ushindi wa mabao 4-2.
 
Bonny akisaidiana na Gervinho kuwania mpira dhidi ya Erasto Nyoni na Nadir Cannavaro wa Taifa Stars

Bao la Bony ndiyo liliivunja nguvu Stars ambayo ilikuwa ikipambana angalau kupata sare ya mabao 3-3, lakini krosi ya Gervinho baada ya kumtoka beki Erasto Nyoni na kipa Juma Kaseja kuipangua, ilimkuta mshambuliaji huyo akiwa peke yake na lango na kufunga kwa ulaini kabisa.

Wakala wake aitwaye, Francis Kacou ameliambia gazeti ala De Gelderlander la Uholanzi kwamba Mwenyekiti wa Swansea, Huw Jenkins ameongeza ofa na wanaweza kukubaliana mara moja kwa kuwa kila kitu kimekwenda vizuri.

Kocha Mkuu wa Swansea, Michael Laudrup ameitaka klabu hiyo kumsajili kwa kuwa mshambuliaji wake huyo ndiyo chaguo lake namba moja katika usajili.


Katika mechi 30 za msimu uliopita akiwa na klabu yake hiyo ya Uholanzi, Bony amefunga mabao 31.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 24, ameichezea Ivory Coast mechi 20 na Laudrup ameonyesha kumtaka bila ya kujali Michu atabaki au kuondoka kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic