Real Madrid imepania kuanza msimu mpya wa 2013-14 kwa kasi kubwa.
Kocha Carlo Ancelotti ametangaza mazoezi yanaanza Jumatatu na wakae wakiamini kazi ni ngumu.
Ancelotti aliyechukua nafasi ya Mourinho amewataka wachezaji hao kumalizia vizuri likizo zao na baada ya hapo ni kazi.
Wachezaji wa Madrid wanasifika kwa kuchati na simu, hivyo inaonekana ni kama sehemu ya onyo kwao kama kazi ikianza, wajue imeanza.
Watakuwa wakifanya mazoezi mara mbili kwa siku, wakianza saa saa 4 asubuhi na baadaye saa 12 jioni.








0 COMMENTS:
Post a Comment