July 10, 2013



 Real Madrid ina mpango wa kutoa ofa kubwa zaidi ya ile iliyotolewa na Arsenal ili kumtwaa mshambuliaji Luis Suarez wa Liverpool.

Madrid imepanga kumwaga pauni milioni 40 ili Suarez raia wa Uruguay atue 'Los Blancos' kwa kuwa watakuwa wameipiku ofa ya Arsenal ambayo ni euro milioni 30.


Mpasha habari amesema Madrid tayari wamewasiliana na wakala wao na huenda ofa yao ikafikia hadi euro milioni 46.

Kikubwa Madrid wanataka kuipiku Arsenal na kumtwaa Suarez na kuna taarifa wamekuwa wakimrubuni asisitize kuondoka Liverpool.
Tayari ameishatangaza anataka kuondoka kwa kuwa msimu ujao anataka kucheza katika timu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya na si kama ilivyo Liverpool.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic