Baba mzazi wa Kiungo nyota wa Yanga, Nizar Khalfan atazikwa leo saa 10 jioni kwenye makaburi ya Mbagala jijini Dar es Salaam.
Khalfan Khalfan amefariki dunia jana jioni katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa.
Nizar amesema baada ya kikao cha pamoja cha wanandugu, wamekubaliana mazishi yafanyike leo.
“Kweli mazishi yatafanyika leo, hivyo tumekuwa tukiendelea na maandalizi,” alisema.
Pamoja na kukipiga Yanga, Nizar amewahi kucheza soka la kulipwa katika nchi za Kuwait, Canada na Marekani.
0 COMMENTS:
Post a Comment