July 21, 2013



 
OGBU (WA PILI KULIA) AKIWA MAZOEZINI YANGA...

Mshambuliaji Mnigeria, Brendan Ogbu anayefanya majaribio katika kikosi cha mabingwa Tanzania Bara, Yanga amesema nusura amwage chozi.

Ogbu amesema alikuwa amepania kucheza mechi ya leo dhidi ya URA ya Uganda angalau kwa dakika 20 lakini imeshindikana kutokana naye kuwa majeruhi.


“Nilitaka kucheza angalau kwa muda huo, kweli nilitaka nionyesha uwezo wangu mapema.

“Lakini nikaona haitawezekana maana kocha alisisitiza lazima niwe fiti,” alisema.

“Awali nilimueleza nilikaa nje ya uwanja kidogo, hivyo sikufanya mazoezi kwa kipindi fulani wakati nikiwa Nigeria.

Mnigeria huyo aliumia wakati akifanya mazoezi na Yanga katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola.

Yeye akataka alazimishe kucheza lakini Kocha Mkuu, Ernie Brandts akamuambia haitawezekana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic