Kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola amesema anajisikia vibaya kutokana na ugonjwa wa kansa unaomsumbua rafiki yake Tito Vilanova.
Vilanova amelazimika kuachia ngazi katika kazi yake ya kuinoa Barcelona baada ya afya yake kuzorota kutokana na ugonjwa wa kansa unaomsumbua.
“Najisikia vibaya sana kuhusiana na Tito, achana na kila kinachotokea lakini ni rafiki yangu ambaye ninampenda kutoka moyoni.
“Bado ninaamini mambo yake yatakuwa mazuri na atarejea katika hali nzuri na mwisho atakuwa katika hali yake ya kawaida,” aliseama.
Hivi karibuni kumezuka hali ya kutoelewana kati ya Guardiola na uongozi wa Barcelona ambao umekuwa ukisisitiza kocha huyo hakuwa na msaada kwa Vilanova.
Vilanova alikuwa msaidizi wa Guardiola wakati akiwa Barcelona na ndiye alipewa jukumu lake baada ya kocha huyo kuachia ngazi na baadaye akaamua kutua Barcelona.
0 COMMENTS:
Post a Comment