July 6, 2013

Bondia aliyekuwa anachipukia kwa kasi katika ngumi za kulipwa, Christopher Mashudu ameuwawa kikatili.

Mashudu,19, umeuwawa kwa kuchomwa visu tumboni na kichwani katika ugomvi ulioibuka juzi katika eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam.

Kocha wa marehemu Mashudu, Christopher Mzazi amethibitisha kuhusiana na tukio hilo na kusema aliyemuua amekimbilia kusikojulikana.

“Kweli ulikuwa ni ugomvi wakati wakiwa katika sherehe, nimeambiwa yule jamaa alimtukana sana marehemu akashindwa kuvumilia.

“Ukaanza ugomvi na marehemu akamzidia jamaa kwa makonde, akakimbia. Wakati watu wanadhani ugomvi ulikuwa umefikia tamati jamaa alirejea tena eneo lile.

“Akaendelea kutamba na Mashudu akainuka wapambane, kumbe jamaa alikuwa ameficha kisu akakitoa na kumchuka mara mbili tumboni na mara moja kichwani akawa amemmaliza kabisa,” alisema Mzazi.

Alisema wanaendelea kushughulikia masuala ya mazishi na Jeshi la Polisi limeahidi kuendelea kumtafuta mtuhumiwa hadi atakapopatikana.
Mashudu alikuwa anapigana katika uzito wa Bantam na alikuwa kati ya wanaochipukia kwa kasi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic