![]() |
| RONALDO (KUSHOTO) AKIFUATIWA NA SHEVCHENKO NA WAZIRI KALADZE WAKIPATA MAELEKEZO KWENYE AKADEMI ALIYOFUNGUA.. |
Mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefungua shule ya michezo maarufu kama ‘akademi’ katika nchini ya Georgia.
Ronaldo alifanya kazi hiyo siku mbili zilizopita baada ya kutua mji mkuu wa nchini hiyo Tbilisi akiongozana na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na AC Milan Andrei Shevchenko na kufanya ufunguzi huo.
Ronaldo alionekana akiwa amevaa fulana nyeupe na kofia na alitumia muda wake mwingi kucheza na watoto katika eneo hilo.
Taarifa zilieleza, Ronaldo ameamua kuanzisha akademi nchini humo baada ya baada ya kualikwa kufanya hivyo na mshambuliaji wa zamani wa AC Milan, Kakha Kaladze ambaye sasa ni Naibu Waziri Mkuu wa Georgia pamoja waziri wa nishati.
Pamoja na kuanzisha Akademi hiyo, Ronaldo alipata nafasi ya kuhudhuria mechi ya kirafiki kati ya Dinamo Tbilisi dhidi ya Dynamo Moscow.
Hivi karibuni, Mreno huyo amekuwa akijihusisha zaidi na masuala ya promosheni, kwani kabla ya Georgia alikuwa nchini Singapore.








0 COMMENTS:
Post a Comment