July 8, 2013



Mshambuliaji wa zamani nyota wa Brazil, Ronaldo Nazario da Lima ameonyesha upendo baada ya kumualika nyota wa Argentina, Lionel Messi katika bonge la pati lililofanyika Sin City nchini Marekani.

Katika pati hiyo, Messi maarufu kama Leo alikuwa njiani kwenda Chicago kwa ajili ya mechi maalum lakini mwaliko huo wa Ronaldo ulimfanya ajumuike naye katika hoteli ya Glitzy hotel.

Ronaldo, mshambuliaji wa zamani wa PSV, Barcelona, Real Madrid na Inter Milan, aliamua kuchagua sehemu hiyo ambayo angeweza kupata sehemu nyingine kama Wynn Las Vegas & Encore Resort, yenye vyumba vya bei nafuu zaidi vinavyoweza kuanzia dola 300.

Messi, ameonekana katika picha mbalimbali akiwa na Ronaldo wanakula bata, lakini pia kaka zake wawili wakubwa wa Messi ambao ni Matías na Rodrigo.

Ronaldo, maarufu kama 'O Fenômeno', ameonekana kuwakuna wengi kutokana na uamuzi wake wa kumulika Messi na kula naye bata pamoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic