July 6, 2013



Yanga imeanza maandalizi ya msimu mpya kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya wakongwe wa soka nchini Uganda Express. Awali Yanga ilipangwa kucheza na mabingwa wa Uganda, KCCA.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza jioni hii, Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao na wakeni hao wakasawazisha.

Bao la mabingwa hao wa Tanzania Bara lilipatikana katika dakika ya 40 mfungaji akiwa ni Hamis Thabit aliyetua Jangwani akitokea African Lyon.
Waganda wakaswazisha katika dakika ya 90 baada ya mabeki wa Yanga kuchelewa kuokoa na Kivumi Winy akasawazisha.

Kikosi cha mabingwa hao kilikuwa hivi: Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Rajab Zahir, Mbuyu Twite, Salum Telela, Nizar Khalfan/Said BahanuzI, HamisI Thabit/Bakari Masoud (Yanga B), Jerry Tegete, Didier Kavumbangu/Sospeter Mhina (Yanga B) na Abdallah Mguli (Yanga B).

Yanga inawakosa wachezaji wake muhimu walio katika kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars inayojiandaa na michuano ya Kombe la Chan.
Timu hizo zinarudiana kesho kwenye Uwanja wa Kambarage katika Manispaa ya Shinyanga.

Maana yake, timu hizo zitalazimika kusafiri kwa muda wa saa mbili na nusu ili kutua Shinyanga kwa ajili ya mechi hiyo ya kesho. Baada ya hapo, safari nyingine itakuwa mjini ambako Yanga itacheza kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Julai 11.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic