July 11, 2013



SUGU (KUSHOTO) AKIWASILI MSIBANI, JAY ANAONEKANA UPANDE WA KULIA..


Mama mzazi wa msanii Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay amefariki dunia kutokana na ajali ya gari.




JAY AKIMPOKEA BABA YAKE MZAZI, MZEE HAULE

Rosemary Manjala amefariki jana usiku na taarifa zinaeleza aligongwa na gari aina ya Toyota Stallet na baadaye kukimbizwa katika hospitali ya Tumbi, Kibaha mkoani Pwani.

“Baada ya ajali mama alinipigia simu, nilikuwa mbali na kuna mtu alifika pale. Lakini ajabu wakaambiwa kwamba alikuwa tayari amepelekwa mochwari, hata mimi sikuamini,” alisema Jay.

Tayari ndugu na marafiki wameanza kukusanyika nyumbani kwa Profesa kuanza taratibu za mazishi na taarifa kamili tutawaletea.
PICHA NA GLADNESS WA GPL

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic