Mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema anataka msimu ujao afunge mabao 70 akiwa na timu yake hiyo.
Ronaldo amesema bila ya kujali kutakuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa Lionel Messi na Neymar wa Barcelona, lakinia nachotaka ni kufunga mabao hayo 70.
Mreno huyo amesema ana uwezo wa kufanya kama atakuwa fiti muda wote na amekuwa akijiandaa vilivyo kuhakikisha anafanikiwa.
Msimu uliopita, Ronaldo alifunga mabao 60 katika mechi za mashindano za Real Madrid na saba wakati timu hiyo ikijiandaa na msimu mpya hivyo kuwa na 67.
Ushindani kutoka kwa Neymar ambaye ametua Barcelona akitokea Santos ya Brazil na Messi lazima utakuwa mkubwa, lakini Mreno huyo anaonekana kutojali.
0 COMMENTS:
Post a Comment