Klabu ya Tottenham iko katika mikakati maalum ya kumbakiza kiungo wake nyota Gareth Bale.
Real Madrid imekuwa ikimtaka kwa udi na uvumba, lakini inaonekana Spurs wanataka kumtumia kwa ajili ya kutangaza jezi zao mpya.
Jezi zao mpya pamoja na mdhamini HP, zinawalazimu kumbakiza Bale ambaye soko lake liko juu.
Kampeni hizo zinaonekana kuanzia kwa wadhamini ambao wanahitaji kupata matangazo ya juu zaidi na wanaona Bale itakuwa ni sehemu ya matangazo hayo kufanya vizuri.
Real Madrid imekuwa ikifanya kila juhudi kumnasa Bale ambaye ni mchezaji bora wa Ligi Kuu England.










0 COMMENTS:
Post a Comment