July 9, 2013



Kipa wa zamani wa Simba, Juma Kaseja amesema ataitangaza timu anayoichezea baada ya kumaliza majukumu ya Taifa Stars.

Kaseja ambaye ni nahodha ataingoza Taifa Stars kuivaa Uganda, The Cranes katika mechi ya kuwania Kombe la Chan kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, Jumamosi.



Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kaseja alisema ni yeye ndiye anajua timu ipi ataichezea msimu ujao na wala si Coastal Union.

“Kila mtu anaweza akasema lake, lakini mimi ndiye nitasema, kama kuhusu Coastal Union watu wamekuwa wakisema tu. Sasa siwezi kuwazuia ila mimi ninajua,” alisema.


“Kwa sasa nisingependa kulizungumzia hilo sana, badala yake acha niangalie zaidi majukumu ya timu ya taifa.”

Simba iligoma kuongeza mkataba na Kaseja kwa madai ameshuka kiwango, lakini Kocha wa Stars, Kim Poulsen amesisitiza Kaseja anaendelea kubaki kipa wake namba moja.

“Namshukuru mwalimu kwa kuniamini, kila mtu anajua mimi ni bora na niliuonyesha ubora wangu tokea nikiwa Moro United, nikacheza Mtibwa Sugar mechi moja.

“Lakini nikaenda Simba, Yanga na baadaye Simba tena na kote nilionyesha ubora. Hivyo naamini yanayotokea sasa yatapita tu.”
Kaseja amchwa Simba akiwa kipa namba moja wa timu hiyo pia nahodha.

1 COMMENTS:

  1. Kaseja ni mtu mzima aachwe afanye maamuzi yake. Kwa uhaini aliofanyiwa na mchango alioutoa Simba mwacheni Kaseja ajitafutie riziki yake

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic