July 13, 2013

Hii ni mechi ya kwanza ya kuwania kucheza fainali za Chan na mechi ya marudiano itachezwa mjini Kampala.
Mshindi kwa jumla ya mechi zote mbili atakuwa amejihakikishia kusonga hadi hatua ya fainali ya michuano ya Chan itakayochezwa nchini Afrika Kusini.
KIPINDI CHA PILI:
Dakika ya kwanza ya mchezo Stars wanashambulia lakini mpira uliporudi tu katika lango la Stars, Uganda wanapata bao kupitia kwa Iguma Denis anayeupiga mpira kiufundi baada ya krosi ya chinichini aliyoiwahi katikati ya mabeki  wa Stars.

 

Hali inavyokwenda, inaonekana Watanzania wanaanza kukata tama, baadhi ya mashabiki wanawazomea baadhi ya wachezaji.
Hata hivyo, Uganda bado wako makini katika kujilinda suala linalosisitizwa na kocha wao Sredojevic Milutin ‘Micho’.
Waganda hao wanaongoza ziada kwa kutumia mtindo wakujiangusha na mara nying wachezaji wao wanajiangusha na kupoteza muda, hali inayowafanya wachezaji wa Stars walalame.
Dakika ya 79 nusura Uganda ipate bao la pili kupitia kwa Frank Kalanda lakini juhudi za Yondani zinasaidia na kuzaa kona lakini inakuwa tasa.
Stars wanaonekana kukata tamaa na tatizo kubwa liko katika upande wa mashambulizi ambayo hayana kasi sana.
Wachezaji wa Uganda wanaendelea kupoteza muda zaidi huku wakiuchukua mpira na kuupeleka katika kibendera kwa ajili ya kupoteza muda.

Viungo wa Stars kama Domayo, Kiemba na Sure Boy wanapoteza mipira sana, hali inayoonekana kuiathiri Stars.

DAKIKA 5 ZA NYONGEZA
Stars wanaonekana kuhaha kutafuta bao, lakini Uganda wanarudisha wachezaji wengi nyuma wakiongozwa na nahodha wao, Hassan Wasswa.
Dalili za kupata zinayeyuka na mashabiki wanaanza kuondoka kwenye majukwaa kuonyesha wamekata tama.
Mpira umekwisha.

Uganda wanaibuka na ushindi wa bao 1-0 na kujipa matumaini zaidi ya kusonga mbele na kucheza Chan nchini Afrika Kusini.
KIPINDI CHA KWANZA:
Mechi kati ya Taifa Stars na Cranes imemalizika katika dakika 45 za kwanza na hakuna timu iliyopata bao.
Inachoonekana Waganda, katika kipindi chote cha kwanza wamecheza kwa kujilinda zaidi huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza.

Hata hivyo, Taifa Stars wanaonekana kucheza kwa kupooza hali inayowafanya mashabiki kuanza kulalamika.

KIKOSI STARS:

Juma Kaseja, Shomari, Kapombe, Nyoni/David Luhende, Agrey Morris, Kelvin Yondani, Frank Domayo, Amri Kiemba, Salum Abubakari, John Bocco, Mwinyi Kazimoto/Haruna Chanongo na Mrisho Ngassa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic