July 12, 2013



 
Kocha mpya wa Bayern Munich, Pep Guardiola amesema anasikitishwa na uongozi wa juu wa Barcelona ambao umeonekana kumtafutia mabaya ili umchafue.

Amesema pamoja na juhudi zake za kutaka waachane naye na kusafiri zaidi ya Kilomita 6,000 nchini Ujerumani lakini bado wamekuwa wakisema maneno mengi ikiwa ni pamoja na kuutumia ugonjwa wa kansa wa Kocha wa Barcelona Tito Vilanova kama fimbo ya kumuumiza na kumchafua.

“Nilishindwa kwenda kumuona Tito kutokana na kubanwa na majukumu wakati akiwa Marekani anatibiwa, lakini sina ugomvi naye hata kidogo kama ambavyo wamekuwa wakisema.

“Inanishangaza sana, wamekuwa wakinishambulia mfululizo bila ya kujali nini kinaendelea. Inawezekana kuhusiana na Neymar, kweli nilimpigia lakini nilianza hivyo miaka mitatu iliyopita baada ya Rais wa Barcelona kuniambia nifanye hivyo ili nimshawishi kama anaweza akajiunga na timu yetu.

“Lakini nilipojiunga na Bayern, nilimpigia tena kutaka kujua kama anataka kuendelea kubaki Brazil au yuko tayari kuja Ulaya. Sasa sijui kama kuna kosa au hilo ndilo jambo la kutafutiana visa,” alilalama Guardiola.

Guardiola amekuwa kocha na mchezaji mwenye mafanikio wakati akiwa BArca na wengi hawakujua kama amekuwa na matatizo makubwa na uongozi wa klabu hiyo kabla ya kuondoka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic