July 1, 2013




Michuano ya vijana chini ya umri wa mika 17 ya Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa imefikia tamati mwishoni mwa wiki kwa timu za Moro Kids, Alliance Schools Academy na Garden kutangazwa mabingwa katika mikoa ya Morogoro, Mwanza na Temeke.

Moro Kids imetwaa uchampioni baada ya kujikusanyia pointi nne sawa na wapinzani wao wakubwa timu ya Techfort lakini Moro Kids wakatangazwa washindi kwa kuwa na magoli mengi ya kufunga. Techfort walihitimisha michuano hiyo kwa kuifunga timu dhaifu ya Anglikana 2-1 katika uwanja wa shule ya sekondari Morogoro. Mabao  yao yalipatikana kupitia kwa washambuliaji Alobogast Mtalemwa na Octatus Lupekenya wakati Anglikana walifunga goli lao pekee kupitia kwa Kessy Khamis.

Hadithi ya mkoani Morogoro vile vile ilitokea huko jijini Mwanza ambapo timu ya Mwanza Alliance Schools Academy ilimemaliza ligi ikiwa na pointi nne sawa na timu ya Marsh Athletical lakini Alliance wakanyakuwa ubingwa wa mkoa kwa kuwa na mabao mengi ya kufunga.

Katika mchezo wa kufunga dimba uliopigwa kwenye uwanja mkongwa wa Nyamagana Ijumaa jioni, Alliance Schools Academy na Marsh Athletical walipambana vikali katika mchezo uliovuta hisia za watazamaji wengi ambapo wachezaji wa pande zote mbili walionyesha vipaji vya hali ya juu ya kusakata kabumbu. 
Mchezo mwingine wa kufunga dimba ulipigwa katika uwanja wa Twalipo katika mkoa wa kisoka wa Temeke jijini Dar es Salaam, ambapo timu ya Garden wallibukwa mabingwa baada ya kuiadhibu bila huruma timu ya Mapambano 4-1. Washindi walipata magoli yao kupitia kwa Badili Salum, Bona David, Juma Masudi na Said Mohamed wakati Mapambano walipaga bao lao la kufutia machozi kupitia kwa Said Hassan.

Wakati huo huo, chama cha soka mkoa wa Morogoro kimetangaza kikosi chake kitakacho uwakilisha mkoa huo katika fainali za taifa za Airtel Rising Stars zinazotarajiwa kuanza kutimua vumbi katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 2 hadi Julai 7.
Kikosi chao kinajumuisha washambuliaji mapacha Evance na Robert Roshan. Wengine ni Fadhili Kamwenda, Juma Shaban, Boniface Myowela, Majid Musisi, Ramadhani Kondo, Rotan Nkamwa, Dickson Mwesa, Alphonce Lukani, Octatus Lupekenya, George Chota, Salum Kiibwa, Shafii Ngesa na Petro Mgaya.
Mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya taifa mwaka huu yanashirikisha timu za wasichana na wavulana kutoka mikoa tisa – Kinondoni, Ilala, na Temeke itakayoleta timu za wasichana na wavulana wakati Tanga, Kigoma na Ruvuma zitashirikisha wasichana pekee huku mikoa ya Morogoro, Mwanza na  Mbeya ikiwa na timu za wavulana tu.

Maandalizi kwa ajili ya mtanange huo wa taifa yamekamilika na timu kutoka mikoani zinatarajiwa kuanza kuwasili jijini Dar es Salaam mwishoni wa wiki tayari kwa mashindano hayo. Fainali za ARS Taifa vile vile zilifanyika katika uwanja huo mwaka jana ambapo Temeke waliibuka washindi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic