July 1, 2013





Mshambuliaji nyota wa Brazil, Neymar amesema siku moja atakuwa ni mwenye furaha sana kama atacheza timu mmoja na Wayne Rooney wa Manchester United.
Neymar amesema kwa kuwa Rooney anaonekana hana raha katika klabu yake, basi afanye mpango wa kuungana naye pamoja na Messi katika kikosi cha Barcelona.

Neymar ambaye amejiunga na Barcelona hivi katibuni kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 48.6 amesema Rooney ni kati ya wachezaji wenye kipaji cha juu duniani.
 
ROONEY AKIWA NA MKEWE COLEEN

Tayari Rooney ameishakutana na kocha wake David Moyes na kujadili kuhusiana na suala la yeye kuomba kuondoka na watakutana tena wiki hii kumaliza kabisa na inaonyesha atabaki Man United.

Jana mshambuliaji huyo aliisaidia Brazil kutwaa Kombe la Mabara huku akiibuka kuwa mfungaji bora katika nafasi ya tatu pia mchezaji bora wa michuano hiyo iliyoisha kwa Brazil kubeba kombe.

Brazil ilibeba kombe kwa kuwachapa mabingwa wa Dunia, Hispania kwa mabao 3-0, moja likiwa limepachikwa kimiani na Neymar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic