Utekelezaji wa amri ya Waziri wa Ujenzi na Miundombinu, John Pombe Magufuri umemuathiri Mlezi wa Simba, Rahma Al
Kharusi maarufu kama Malkia wa Nyuki baada ya moja ya ofisi zake jijini Dar es
Salaam kubomolewa.
Ofisi hiyo
ambayo ilikuwa inaendesha shughuli za kampuni ya kuuza mafuta ya RPB Oil
inayomilikiwa na Malkia wa Nyuki imepobomolewa.
Bomoabomoa
hiyo ya Magufuri imepamba moto katika Barabara ya Old Bagamoyo na majumba
kadhaa yamepobolewa kwa kuwa kuna ujenzi wa kuitanua barabara hiyo.
Ofisi ya
Malkia wa nyuki ilikuwa katika ghorofa ya kwanza ya jengo la Green Acres,
katikati ya makumbusho na Victoria na imevunjwa.
Ingawa
jengo hilo halijavunjwa lote, lakini sehemu ya ofisi ya RPB Oil iliyokuwa
upande wa barabarani imebomolewa yote.
Malkia wa
nyuki ndiye mwanamama aliyetikisa katika soka mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kuilipia Simba zaidi
ya Sh milioni 70 kwenda kuweka kambi nchini Oman.
Lakini
akalipa tena zaidi ya Sh milioni 50 kumpa kocha Milovan Cirkovic aliyekuwa anaidai
Simba bila ya mafanikio. Baada ya hapo, Malkia wa nyuki amekuwa kimyaa na
mashabiki wengi wamekuwa wakihoji kutaka kujua aliko.
Taarifa
zinaeleza yuko nchini Oman anakoendelea na biashara zake, lakini ndugu yake
mwingine alisema amebanwa majukumu ya makampuni yake nchini Marekani.
0 COMMENTS:
Post a Comment