TWITE (KULIA) AKIWA MAZOEZINI YANGA, WIKI ILIYOPITA.. |
NA SALEH ALLY
Majanga kwa
Yanga kwa kuwa huenda beki wao nyota, Mbuyu Twite atalazimika kupumzishwa kwa
zaidi ya mwezi mmoja.
Twite raia
wa Rwanda mwenyea sili ya DR Congo, huenda akapumzishwa kwa kuwa analazimika
kufanyiwa upasuaji wa mguu ili kuondoa chuma kilicho mguuni mwake.
Uamuzi wa
kuondoa chuma hicho umetokana na Twite kupata uvimbe nyuma ya goti lake na
wataalamu wanaeleza unatokana na chuma kilicho katika mguuni mwake.
Twite
amecheza na chuma hicho kwa zaidi ya miaka minne baada ya kuwekewa kutokana na
kuvunjika mguu akiwa uwanjani.
Pamoja na
kusuasua kuelezea kuhusiana na suala hilo, baadaye Daktari wa Yanga, Nassor
Matuzya alisema wako katika mchakato wa kulishughulikia suala hilo.
“Hakika
sikutaka kusema kuhusiana na suala hilo, lakini lisichukuliwe kama kubwa sana,
ila kweli Twite ana tatizo na mguu wake umekuwa ukivimba nyuma ya goti kila
anavyofanya mazoezi makali.
“Sasa
nimemsimamisha kufanya mazoezi, kesho (leo) tutaenda kwa daktari bingwa wa
magonjwa yanayohusiana na michezo naye atatushauri, nafikiri ndiyo msaada
ninaohitaji lakini kwa kuangalia tu inawezekana akafanyiwa upasuaji,” alisema
Matuzya na alipoulizwa ikiwa ni upasuaji atakaa nje kwa muda gani.
“Inaweza
kufika mwezi mmoja au zaidi, lakini suala hilo linashughulikiwa kwa ukaribu
kabisa na uongozi unafuatilia.”
Pamoja na
Matuzya kutotaka kuelezea zaidi, chanzo cha ndani kutoka Yanga kimeeleza Twite
atafanyiwa upasuaji ili kuondoa chuma hicho kwa lengo la kuepusha uvimbe huo
kuendelea.
Chuma hicho
kiliwekwa kumsaidia kurejea katika hali yake na kutokana na hali inavyokwenda,
inaonekana hakuna ujanja, lazima kitolewe lakini upasuaji lazima ufanywe na
daktari bingwa.
Beki huyo
alijiunga na Yanga msimu uliopita akitokea APR ya Rwanda, kabla ya hapo, Simba
walimtangaza kuwa atatua Msimbazi na mwenyeki, Ismail Aden Rage akapiga naye
picha na kuitupia Facebook, lakini siku chache mambo yakageuka.
0 COMMENTS:
Post a Comment