July 21, 2013




Kocha Gerardo ‘Tata’ Martimo ndiye anaonekana ana nafasi kubwa ya kuchukua nafasi ya Kocha Mkuu wa Barcelona iliyoachwa na Tito Vilanova anayesumbuliwa na maradhi ya kansa.

Tata raia wa Argentina ambaye anaifundisha Newell Old Boys iliyomlea Messi ndiye anapwa nafasi hiyo na Barcelona wameanza mazungumzo naye.

Taarifa zimeeleza Bosi ya Barcelona aliyeishughulika na masuala ya usajili, Andoni Zubizerreta na Raúl Sanllehí watasafiri hadi mji mkubwa zaidi wa Argentina, Buenos Aires kufanya mazungumzo na Tata.



Wawili hao wanatarajia kuondoka usiku huu kwenda kuzungumza na Tata kwa ajili ya kwenda Barcelona na kuanza kasi.
Taarifa zinaeleza Messi amekuwa akitia chumvi ili kuhakikisha Barcelona inamata kocha huyo kwa ajili ya kazi hiyo ngumu.

Wakati akiinoaNewells Old Boys ilisifika kwa kuwa timu yenye soka la kuvutia, kasi na uhakika na alikuwa akiwaniwa na timu nyingi za Amerika Kusini na mara nyingi alikataa kuondoka nchini Argentina.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic