Mabingwa wa England, Manchester United wamemaliza mazoezi yao nchini Australia kwa kujifua ufukweni.
Mazoezi hayo ya ufukweni hayakuwa magumu sana na baada ya hapo inafuatia mipango ya safari kwenda nchini Japan.
Kocha Mkuu, David Moyes alisema baada ya mazoezi hayo katika ufukwe wa Bondi, akili yao wanaelekeza nchini Japan.
Wakiwa nchini Japan, Man United watawavaa Yokohama F-Marinos, Jumanne ijayo mjini Yokohama.
Hiyo ni kati ya mechi tano ambazo Man United watacheza katika kipindi hicho cha ziara ya kujiandaa na msimu mpya.
0 COMMENTS:
Post a Comment