Hatimaye Real Madrid imempata mnunuzi wa Gonzalo Higuaín baada ya timu kutoka Serie A kukubali kumwaga kitita cha euro milioni 35.
Watukutu wa Napoli ndiyo wamekubali kutoa fedha hizo na kumsajili Higuain ambaye alikuwa anawaniwa kwa udi na uvumba na Arsenal ya England.
Mara ya mwisho, Arsenal walitangaza kuwa katika hatua za mwisho kumnasa Higuain na mwisho walikuwa wamekubali kutoa euri milioni 27.
Hata hivyo, bado Real Madrid wala Napoli hakuna aliyetangaza kuhusiana na kukubaliana kwao kuhusiana na usajili huo na inaonekana watafanya hivyo kama malipo yatafanyika.
Lakini mwisho inaonekana Napoli wamewazidi dau kwa mbali na kumchukua Muargentina huyo.
Inaonekana Napoli kwa haraka wamekuwa wateha wazuri wa Real Madrid baada ya kununua wachezaji wawili kabla ya Higuain wakianza na Callejón (€10m) na Albiol (€11m).
0 COMMENTS:
Post a Comment