July 21, 2013



Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amesema sare dhidi ya URA ya Uganda ina faida kubwa kwao.

Yanga walilazimika kusawazisha katika dakika za mwisho ili kupata sare ya mabao 2-2 dhidi ya URA. Bao la pili lilifungwa na Jerry Tetege wakati lile la kwanza ambalo lilikuwa la kusawazisha pia lilifungwa na Dider Kavumbagu.



Brandts amesema pamoja na kukosa lundo la wachezaji walio katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars, amefanikiwa kuona baadhi ya wachezaji ambao huenda wasingepata nafasi.

“Tumepata kitu kikubwa sana ambacho naona ni bora zaidi ya kuangalia matokeo pekee ya sare.


“Mfano bao la kusawazisha la Jerry (Tegete), watu waliisha kata tamaa na inaonyesha kawaida sisi tunapigana hadi mwisho.

“Lakini hatuna wachezaji zaidi ya wanne walio katika kikosi cha timu ya taifa na tumeweza kufanya vizuri,” alisema Brandts.

Hata hivyo alikubali kikosi chake hakikucheza katika kiwango kizuri ukilinganisha na URA.

“Kidogo hapa nalazimika kufafanua, utaona Yanga imejaa sura mpya na sasa tunafanya kazi ya kuunda timu, lakini URA wanaendelea na ligi, maana yake ni timu ambayo iko katika mwendo. Lazima kuwe na tofauti,” alisema.


URA tayari wamecheza mechi mbili, mechi ya kwanza jana walianza kwa kuichapa Simba kwa bao 2-1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic