OWINO WAKATI AKIWA SIMBA |
Uongozi wa
URA ya Uganda umecharuka na kusema unashangazwa na kuiona inamtaka beki Joseph
Owino.
Meneja wa
URA, Sam Okabo amesema Simba walimuona mchezaji huyo kama takataka wakati akiwa
mgonjwa.
“Tunashangazwa
kuona wamekusanyika na kumpapatikia, wanataka kumsajili tena. Hadi sasa Owino
ni mali yetu.
“Tungependa
wafuate utaratibu lakini si kuanza kuzungumza tu na mchezaji kwanza hata kama
atakuwa na mkatana mfupi na sisi,” alisema Okabo.
Simba
ilimuacha Owino ikiwa ni siku chache baada ya kubadilishana na Uhuru Selemani
ambaye alikwenda Azam FC.
Lakini ikaonekana
alikuwa hajapona vizuri hivyo viongozi wa Simba wakaamua kuachana naye na
kuanza kuhaha kusaka mabeki wengine.
Mwenyekiti wa
Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope alimfuata Owino baada ya mechi
ya kirafiki dhidi ya URA ambayo Msimbazi walilala.
0 COMMENTS:
Post a Comment