July 22, 2013



 



Mkurugenzi wa Ufundi wa Coastal Union, Mohammed Bin Slum alionyesha ni mzazi na rafiki wa kweli baada ya kutumia dakika kadhaa akitoa nasaha kwa kiungo wa Yanga, Nizar Khalfan.

Bin Slum alifanya hivyo jana alipokwenda kushiriki mazishi ya baba mzazi wa Nizar, Khalfan Khalfan.



Akiwa nyumbani kwao Nizar, Mbagala jijini Dar es Salaam, Bin Slum alifanya kazi ya ziada kuzungumza na Nizar aliyekuwa akilia kwa uchungu.
Alionyesha kumuelezea kuhusiana na matatizo ya kufiwa, pia alimfariji na baadaye mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Idd Moshi ‘Mnyamwezi’ naye akafanya hivyo.

Wakati wawili hao wakifanya hivyo, Razack Khalfan, mdogo wa Nizar na kiungo wa Coastal Union, alikuwa akisikiliza kwa umakini mkubwa.
Watu mbalimbali walijitokeza kumpa pole Nizar na Khalfan na kikosi kizima cha Yanga kikiongozwa na Kocha Ernie Brandts kilifika kwao na baadaye katika mazishi.
Mwenye Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya wetu, Khalfan Khalfan.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic