Gerardo 'Tata' Martino ndiye kocha mpya wa Barcelona aliyechukua nafasi ya Tito Vilanova.
Tata amesaini mkataba wa miaka mitatu kuinoa Barcelona na imeelezwa tokea awali alikuwa anapigiwa debe na Lionel Messi.
Raia huyo wa Argentina aliyewahi kuinoa Newell's Old Boys, timu iliyomkuza Messi kisoka, anasifiwa kwa kufundisha soka na kuvutia.
Tata amepewa nafasi hiyo kutokana na Vilanova kulazimika kupumzika kutokana na ugonjwa wa kansa unamkabili kufanya afya yake kuzorota zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment