Uuongozi wa
klabu ya Simba umepanga kufanya mkutano mkuu wa mwaka Julai 20 kwenye ukumbi
wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oystrebay, Dar es Salaam.
Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang’are al maarufu kama Mzee Kinesi amesema muda mchache uliopita kwua wamekubaliana hilo katika kikao kilichofanyika jana usiku.
Kinesi
amesema wamekuwa wakiendelea na mkutano huo pamoja na mchakato mzima wa zoezi
la mkutano huo wa kikatiba.
Alisema mambo kadhaa
muhimu kuhusiana na klabu hiyo ikiwa ni pamoja na mwenendo wa Simba
yatajadiliwa.
Lakini suala
la ombi la kujiuzulu kwa Geofrey Nyanga ‘Kaburu’ ambaye Mzee Kinesi anakaimu
nafasi yake pia litajadiliwa.
Pamoja na
hivyo, kumekuwa na taarifa ya hofu kwa baadhi ya wanachama wa Simba ambao
wamekuwa wakieleza kuwa kuna harufu ya mabadiliko ya katika yanayolenga
kufaidisha watu wachache.
Wanachama hao
wamekuwa wakidai viongozi wanataka kufanya mabadiliko kwa ajili ya kujinufaisha
wao na wanachama wanapaswa kuwa makini.
Hata hivyo
uongozi wa Simba umesisitiza unafanya mambo yote kwa ajili ya manufaa ya klabu
na si kujinufaisha kama ambavyo baadhi ya wanachama wameanza kupata hifu.
0 COMMENTS:
Post a Comment