NIYONZIMA (KULIA) AKIWANIA MPIRA NA HAMIS KIIZA KATIKA MOJA YA MAZOEZI YA YANGA MSIMU ULIOPITA. |
Baada ya ukimya, hatimaye imejulikana sababu za kuchelewa kwa kiungo
nyota wa Yanga, Haruna Niyonzima.
Niyonzima ameshindwa kujiunga na wenzake baada ya kununua nyumba
ambayo imeingia katika mgogoro nchini kwao Rwanda.
Awali uongozi wa Yanga ulisema ulikuwa ukimtafuta Niyonzima bila ya
mafanikio, hivyo haukuwa ukijua sababu za msingi za yeye kuchelewa.
Lakini baadaye Niyonzima alimpigia kocha wake Ernie Brandts kwamba ni
lazima alimalize tatizo hilo kabla ya kurejea nchini.
Salehjembe liliamua kuwasiliana na Brandts ili kujua ukweli kuhusiana
na kiungo huyo kwa kuwa awali alionyesha kukasirishwa na kitendo hicho cha
uchelewaji kama ilivyokuwa kwa kiungo wake Athumani Idd ‘Chuji’ na Kelvin
Yondani ambayo hawakutokea mazoezini, siku ya kwanza.
“Kweli nimewasiliana na Niyonzima na ana matatizo ambayo anatakiwa
kuyamaliza,” alsiema Brandts.
Alipoulizwa kama ni suala lipi hasa ambalo limemkwamisha, alisema: “Kweli
linahusiana na manunuzi ya kitu, lakini vizuri ujue kwamba ana tatizo hilo na
akimaliza atakuja na sasa nimekuwa nikiwasiliana naye ili kujua maendeleo.”
Imeelezwa Niyonzima aliuziwa nyumba ambayo tayari alikuwa ameuziwa mtu
mwingine, hivyo kusababisha kuzuka kwa mgogoro huo.
Lakini mmoja wa marafiki wa Salehjembe
ambaye ni mwandishi wa habari mjini Kigali, alisema nyumba aliyouziwa
amegundua baadaye ina mgogoro.
“Lakini suala lake limekuwa likifanywa ni siri kubwa na halijafikia
wmafaka,” alisema.
Rwanda ni kati ya nchi zinazofuata sana mkondo wa sheria, hivyo
inaonekana suala hilo lazima litapata ufumbuzi ndani ya siku chache.
0 COMMENTS:
Post a Comment