![]() |
| AL FAYED, MMILIKI WA ZAMANI WA FULHAM AKIWA KARIBU NA SANAMU LA MICHAEL JACKSON.. |
Mmiliki mpya wa klabu ya Fulham, bilionea Shahid Khan ameonywa mapema kuwa makini kabla ya kuchukua uamuzi wa kuliondoa sanamu la Michael Jackson.
Sanamu hilo la msanii huyo maarufu zaidi wa Marekani ambaye sasa ni marehemu limewekwa kwenye jengo la Fulham na kulikuwa na taarifa kwamba Khan kutoka Marekani angeweza kulitoa.
![]() |
| AL FAYED AKIWA NA KHAN AMBAYE NI MMILIKI MPYA |
Pamoja na kuonywa na mashabiki, lakini aliyekuwa mmiliki wake, Mohamed Al Fayed pia amemtaka Khan kuwasilikiza mashabiki kabla ya kuchukua uamuzi.
Amemwambia sanamu hilo waliloliweka mwkaa 2001, ni sawa na mali ya mashabiki na wanataka kushirikishwa kabla ya uamuzi wa kuliondoa.
Fayed, 84 alisema
ana uhakika klabu hiyo aliyoiuza kwa pauni milioni 200 imepata mtu sahihi
ambaye ataiendeleza vizuri na kufanya mambo kwa ufasaha.
Kwa upande wa
Khan naye amesisitiza kwamba atahakikisha anaheshimu historia ya klabu hiyo na
kuendeleza mazuri ya Al Fayed aliyeimiliki klabu hiyo kwa miaka 16.









0 COMMENTS:
Post a Comment