July 9, 2013



Jose Mourinho ameanza kazi Chelsea akionyesha kuwa mambo yanabadilika kutokana na wakati.

Badala ya kutumia kitabu au daftari, safari hii Mourinho amekuwa akitumia iPad kutoa maelekezo kadhaa kwa wachezaji.

Pamoja na kutoa maelekezo hayo, ili kuonyesha yuko tofauti na makocha wengine, Mourinho amekuwa akitumia muda wake mwingi kusoma katika iPad yake hiyo.

Kocha huyo leo asubuhi alifanya mazoezi kwa zaidi ya saa moja na nusu akionyesha kuwa kazi imeanza na anachotaka ni ubingwa.

Mourinho ametua Chelsea kwa mara nyingine akitokea Real Madrid ambayo alijiunga nayo akitokea Inter Milan ya Italia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic