Timu ya Simba inatarajiwa
kwenda Kisumu, Kenya Julai 31 kushiriki Michuano ya Kilimo yatakayofanyika
nchini humo baada ya kukamilika ziala yao ya Tabora, Musoma, Mwanza
watakapokwenda kucheza mechi za kirafiki.
Kabla ya kwenda Kenya,
Simba itakuwa na safari ya kuelekea Katavi walipopata mwaliko kutoka kwa Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda kucheza mechi ya kirafiki mkoani humo ambapo wanatarajia
kuondoka Julai 13.
Akizungumza na Championi
Ijumaa, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema, ziara hizo zitakuwa ni
moja ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu.
“Tunatarajia kufanya
ziara ya kutembelea sehemu mabli mbali ili kuweza kujiandaa na msimu mpya wa
ligi kwa kwenda, Kenya, Katavi, Musoma, Tabora na Mwanza.
“Pia tutakuwa na ziara ya
kijamii kwa kutembelea vitua vya watoto yatima ikiwa ni pamoja na kuandaa siku
ya Simba day Agosti 8 na kuhudhuria semina ya wadahamini wetu TBL kabla ya ligi
kuanza,” alisema Kamwaga.
Alimalizia kwa kusema,
wakati timu ya wakubwa ikiendelea na ziara yake hiyo kikosi cha timu B
kitakwenda jijini Arusha kushiriki michuano ya Rolingstone.
0 COMMENTS:
Post a Comment