July 5, 2013



 Uongzoi wa Klabu ya Simba umeamua kumuongeza mkataba mwingine aliyekuwa Ofisa Habari wake, Ezekiel Kamwaga kwa lengo la kuitumikia tena.

Awali, Kamwaga alitangaza kumwaga manyanga kuitumikia klabu hiyo baada ya mkataba wake kufikia tamati mapema mwezi Mei.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala alisema kuwa tayari wameshamalizana na Kamwaga.

“Tumeshamuongeza mkataba Kamwaga, hivyo ataendelea kuwa msemaji wa Simba. Kilichotokea awali ni mkataba wake kwisha tu,” alisema Mtawala.
SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic