July 23, 2013




Klabu ya Simba imesema inaonekana hakuna nafasi kwa mabeki wawili Waganda, Hamis Buyinza na Samuel Ssenkoomi na badala yake Joseph Owino ndiye chaguo lao.

Simba tayari imeanza mazungumzo na Owino ambaye alikuwa beki wake kabla hajajiunga na Azam FC huku akiondoka Simba na kulaumu walishindwa kumtibu baada ya kuumia.

Simba ilivutiwa tena na Owino baada ya kumuona akicheza mechi mbili za kirafiki akiwa na URA ambayo ilizivaa Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope amethibitisha kuhusiana na Owino.



“Kweli tuko katika mazungumzo na kama mambo yatakwenda vizuri tutamsajili. Owino amekuwa ni pendekezo namba moja la benchi la ufundi.
“Kuhusiana na Ssenkoomi na Buyinza, hawa walipewa nafasi ya benchi la ufundi lakini linaonekana kutofurahishwa nao. Hivyo sisi hatuna namna,” alisema Hans Pope.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic