Kocha Mkuu wa Uganda, The Cranes, Sredojevic Milutin amesema amewaonya wachezaji wake kuidharau Taifa Stars katika mechi yao ya marudiano wikiendi hii mjini Kampala.
The Cranes inapambana na Stars kuwania kucheza fainali za Chan zilizopangwa kucheza nchini Afrika Kusini.
Milutin maarufu kama Micho amesema wachezaji wake wanapaswa kuwa makini sana kwa kuwa Taifa Stars haitakuwa na la kupoteza.
“Nimewaambia namna watakavyojituma na hawana cha kupoteza, lazima watataka ushindi na presha kubwa itakuwa kwetu.
“Kweli tutapambana vilivyo na nimewaonya kama wakitanguliza dharau tunaweza kuanguka tukiwa nyumbani,” alsiema.
Katika mechi ya kwanza, Stars ililala kwa bao 1-0 jijini Dar es Salaam, inatakiwa kushinda kuanzia mabao 2-0 kwenda mbele ili isonge.
Stars iko kambini jijini Mwanza na inatarajia kuondoka nchini kesho kwenda Uganda kwa ajili ya pambano hilo.
Kocha Mkuu, Kim Poulsen alisema wamejiandaa vilivyo ili kushinda pambano hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment