Wakati inaonekana kama mambo yamepoa, wakala wa Gareth Bale amefikia makubaliano na Rais wa Real Madrid, Florentino Perez ya mshahara wa euro milioni 10 wa winga huyo mwenye kasi.
Daniel Levy amesema anaendelea kufanya makubaliano hayo kwa kuwa Bale alimuambia alitaka kucheza Real Madrid tokea akiwa mtoto na hatakubali kuipoteza nafasi hiyo.
Levy amesema anaamini Madrid wanaweza kumlipa kila anachotaka anachana na kwamba mwaka 2009 walitoa pauni milioni 80 kumtwaa Cristiano Ronaldo, lakini bado wanamhitaji Bale na hawatanii katika hilo.
Alisema awali mshahara wa Bale ulifikia euro milioni 7 kutoka sita kwa mwaka, lakini sasa imepanda na kufikia euro milioni 10, kitu anaona ni kizuri kwa Bale.
Hivi karibuni, Kocha wa Tottenham Hotspurs, AVB alisema Bale hataondoka na kusisitiza ameishalimaza suala hilo.
Lakini Madrid wanaonyesha hawajamaliza na hasa kutokana na presha wanayoipata kutokana na kuhamia kwa Neymar kwa wapinzani wao Barcelona.
0 COMMENTS:
Post a Comment