| KIEMBA (KULIA) AKIWA MAZOEZINI SIMBA |
Ndoto za kiunyo nyota wa Simba, Amri Kiemba kucheza
soka la kulipwa nje ya Tanzania, zimeanza kuingia doa.
Inaonekana timu zilizokuwa zinamtaka kutoka katika
nchi za Israel, Ureno na Morocco zimesitisha zoezi hilo na chanzo kimeelezwa
kuwa umri.
Timu ya Raja Casablanca ya Morocco ndiyo ilikuwa
ikienda kasi kutaka kumnasa Kiemba, lakini mambo yamekuwa tofauti.
Awali timu hiyo ilikuwa tayari kutoa hadi dola 150,000
lakini Simba ikaona ni kiasi kidogo.
Alipoulizwa juu ya taarifa hizo, Mwenyekiti wa Kamati
ya Usajili ya Simba, Zakaria Hans Pope alisema imekuwa vigumu kwa mchezaji huyo
kuweza kupata timu kirahisi kutokana na umri wake kumtupa mkono.
“Siyo lahisi kupata timu haraka kwa Kiemba kufuatia
umri wake kuwa mkubwa, kwani kwa sasa ana miaka 30, hivyo kufanya klabu ziweze
kusuasua katika suala zima la kumsajili.
“Kwa sasa bado tunaendelea na maongezi na klabu hizo
na iwapo tutafikia makubaliano basi atakwenda,” alisema Hans Pope.
Hivi karibuni, Kiemba alisaini mkataba mpya wa
kuendelea kuitumikia Simba kwa dau la shilingi milioni 35, licha ya kuwa Yanga
nayo ilikuwa ikimuwania.







0 COMMENTS:
Post a Comment