STARS AMBAYO ITAKWENDA KAMPALA BILA SAMATTA NA ULIMWENGU |
Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa
Stars inaondoka Mwanza keshokutwa kwenda Kampala, Uganda
kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la CHAN itakayochezwa Jumamosi (Julai
27 mwaka huu) Uwanja wa Mandela kuanzia saa 10 kamili jioni.
Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Mwanza chini ya Kocha Kim Poulsen
tangu Julai 14 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo itakayoamua ni timu ipi kati
ya hizo mbili itacheza Fainali za CHAN zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Timu hiyo itaondoka Uwanja wa Ndege
wa Mwanza saa 7.25 mchana kwa ndege ya PrecisionAir, na inatarajiwa kutua
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 10.15 jioni.
Wakati huo huo, Kocha Kim Poulsen
kesho (Julai 23 mwaka huu) atakuwa na mkutano na waandishi wa habari
kuzungumzia maandalizi ya kikosi chake. Mkutano huo utafanyika saa 5 kamili
asubuhi kwenye hoteli ya La Kairo jijini Mwanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment