Shirikisho la Soka Afrika
(Caf) limeteua waamuzi kutoka Burundi kuchezesha mechi ya kwanza ya mchujo ya
Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (Chan) kati ya Tanzania, Taifa
Stars na Uganda, The Cranes itakayofanyika Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Waamuzi hao ni Thierry Nkurunziza
atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake watakuwa Jean Claude Birumushahu na
Pascal Ndimunzigo. Mwamuzi wa akiba (fourth official) ni pacifique
Ndabihawenimana.
Kamishna wa mechi hiyo Gebreyesus
Tesfaye kutoka Eritrea. Tesfaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Eritrea na
mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya Chan.
The Cranes inanolewa na Kocha Mserbia, Milutin
Sredojevic ‘Micho’ aliyewahi kuinoa Yanga na baadaye timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’.
Wakati huo huo, Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limeteua
Leslie Liunda wa Tanzania kuwa Kamishna wa mechi kati ya Burundi na Sudan
itakayochezwa jijini Bujumbura.
Mechi
hiyo ya kwanza ya mchujo ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani
(Chan) itafanyika keshokutwa (Julai 7 mwaka huu). Liunda anatarajia kuondoka
leo usiku (Julai 5 mwaka huu) kwenda Bujumbura.







0 COMMENTS:
Post a Comment