![]() |
| RAIS KIKWETE AKICHEZA MPIRA NA MGENI WAKE RAIS WA MAREKANI BARACK OBAMA, WIKI ILIYOPITA JIJINI DAR |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la
Matumaini ambalo litafanyika kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam.
Mbali na kuwa mgeni rasmi, Rais Kikwete
ambaye ni mdau mkubwa wa michezo ya soka na kikapu, anatarajiwa kuwa mwamuzi wa
mchezo wa soka ambao utawakutanisha Wabunge wa Simba watakaopepetana na wenzao
wa Yanga, ikiwa ni sehemu ya tamasha hilo.
Mratibu wa tamasha hilo ambalo
linafanyika mara moja kwa mwaka, Abdallah Mrisho amesema kuwa Rais Kikwete
amekubali kuwa mgeni rasmi ambapo tachezesha mechi hiyo lakini pia atatoa neno
la matumaini mwa maelfu ya watu watakaojitokeza uwanjani hapo.
Akizungumzia zaidi Mrisho anasema:
“Rais Kikwete amekubali ombi letu la kuwa mgeni rasmi, pia atashika kipenga na
kuchezesha mechi ya Wabunge kwa dakika kadhaa, ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa
mechi hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa.”
Katika tamasha hilo kutakuwa na
burudani na michezo mbalimbali ambapo litaanza saa nne asubuhi na kufikia
tamati saa sita usiku.
“Mchezo mwingine wa siku hiyo
utakuwa kati ya Bongo Fleva dhidi ya Bongo Muvie, burudani nyingine ni pambano
la ndondi kati ya mwigizaji Aunt Ezekiel dhidi ya Mbunge Ester Bulaya, staa mwingine
wa filamu Jacqueline Wolper atapigana na Mbunge Halima Mdee, Mbunge Zitto Kabwe
atachapana na Vincent Kigosi ‘Ray’,” alisema Mrisho na kuendelea:
“Mbali
na mapambano hayo ya burudani, kutakuwa na mapambano ya ukweli kati ya Francis
Miyeyusho dhidi ya Shadrack Muchanje, Thomas Mashali dhidi ya Patrick Amote.”
Mrisho aliongeza kuwa kutakuwa na
burudani ya wanamuziki wengi, baadhi yao ni rapa wa Kenya, Jackson Makini
‘Prezzo na Nasib Abdul ‘Diamond’.








0 COMMENTS:
Post a Comment