July 10, 2013




Ndani ya saa 48 zijazo, klabu ya Southampton ya England inatarajia kunasa kiungo Mkenya, Victor Wanyama raia wa Kenya.

Southampton imekubali kumchukua Wanyama kwa dau la pauni milioni 12.5 ambalo limeweka rekodi ya mauzo kwa klabu hiyo ya Scoltland.

Mwaka 2010, Celtic ilimuuza Aiden McGeady kwa Spartak Moscow kwa kitita cha pauni milioni 11 kilichokuwa kinashikilia rekodi ya mauzo.

Kaka yake Wanyama, MacDonald Mariga ni kiungo nyota wa AC Milan ya Italia ambayo imempeleka kwa mkopo Parma.

 
Tayari Wanyama ,22, amewaambia rafiki zake wa karibu kwamba huenda akawaaga wachezaji wenzake na kocha wake Neil Lennon katika uwanja wao wa mazoezi katika eneo la German katika kipindi kifupi kijacho.

“Wanyama yuko katika hatua za mwisho kuondoka Celtic na anajiunga na Southampton,” alisema mmoja wa rafiki zake wa karibu.

Wanyama alijiunga na Celtic miaka miwili iliyopita kwa dau la pauni 900,000 akitokea Beerschot ya Ubeligiji.

Maana yake Celtic itakuwa imefanya boashara ya maana kwa mchezaji huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic