August 2, 2013



BEKI wa kimataifa wa Yanga, Mbuyu Twite, leo Ijumaa anatarajiwa kufanyiwa uangalizi wa awali wa kitabibu juu ya uvimbe uliojitokeza nyuma ya goti kabla ya kufanyiwa uchunguzi wa kina kesho Jumamosi kwenye Hospitali ya Sanita, Mikocheni jijini Dar.
Twite ambaye alibainika kuwa na chuma katika mguu wake ambacho amecheza nacho kwa zaidi ya miaka minne baada ya kuwekewa kutokana na kuvunjika mguu akiwa uwanjani, ataendelea kubaki nacho kwa kuwa ndicho ambacho kinamwezesha kuwa fiti kwa mujibu wa dakatari wa klabu yake.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Daktari wa Yanga, Nassor Matuzya alisema madaktari wa Ami Trauma Center iliyopo Msasani walimfanyia uchunguzi wa awali na kudai kuwa wanahitaji kumchunguza tena ili kujua ni nini kilichosababisha uvimbe huo kutokea.

“Chuma alichowekewa hakiwezi kutolewa na siyo tatizo kuwepo mwilini mwake kwa kuwa ndicho kinachomsaidia mguu wake kufanya kazi,” alisema Matuzya.

Alisema maendeleo yake mpaka sasa ni mazuri lakini yupo kwenye uangalizi mpaka leo Ijumaa. Akasisitiza kuwa Twite amekuwa akitaka kuendelea na mazoezi lakini alimzuia kwa kuwa anataka kulimaliza kabisa tatizo hilo kabla ya ligi kuanza.

 Habari: Lucy Mgina na Martha Mboma



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic