Na Mwandishi
Wetu
MABOSI wa
Klabu ya Yanga na wale wa Kampuni ya Azam, wamekutana kwa siri katika
kujadiliana juu ya sakata la Yanga kugomea mchakato wa kuonyeshwa kwa michezo
yao ya Ligi Kuu Bara.
Kiongozi wa
juu wa Yanga ameliambia gazeti hili jana kuwa wameshapeleka barua hiyo na
wanangoja utekelezaji.
Lakini
wakati huohuo, uamuzi wa kukutana kwa viongozi wa Yanga na wale wa Kampuni ya
Azam inakuwa ni muendelezo wa sakata zito lililopo sasa, ambapo Yanga wamekuwa
wakigomea mchakato wa kampuni hiyo kuonyesha michezo yao kutokana na Yanga
kutokukubali kiasi cha Sh milioni 100 walizotakiwa kulipwa na Azam.
Taarifa
ambazo Championi Ijumaa limezipata, zimedai kuwa viongozi wa juu wa Yanga
walikutana na bosi mmoja wa Azam kujadiliana juu ya sakata hilo ingawa vikao
hivyo havikumalizika kwa muafaka.
Mmoja wa
mabosi wa Kampuni ya Azam amesema viongozi hao walikutana na bosi wa kampuni
hiyo ambapo Yanga walizungumzia juu ya kutaka kulipwa zaidi ya klabu nyingine,
hoja ambayo bosi huyo wa Azam alionyesha kukaribia kuikubali, ingawa alishindwa
kuwapa jibu la moja kwa moja akiwataka kumpa muda.
“Hatuna
tatizo na Yanga katika hili, ndiyo maana na hata bosi wetu (anamtaja kwa jina)
alikubali kukutana na viongozi wa juu wa klabu hiyo, ingawa walishindwa
kuafikiana katika vikao viwili tofauti walivyovifanya,” alisema mmoja wa
viongozi wa Klabu ya Azam.
0 COMMENTS:
Post a Comment