HUMUD AKIWA MAZOEZINI SIMBA.. |
Ingawa bado haijapitishwa hadharani lakini mjadala mkubwa umezuka ndani ya klabu ya Simba kuhusiana na kiungo Abdulhalim Humud.
Uamuzi wa kwamba ajisajiliwe umepitishwa ingawa inaonekana kuna upande unaonekana kumhitaji.
Lakini watu wengi wanaohusika kamati ya ufundi na hata sehemu ya benchi la ufundi litaka kiungo huyo aachwe.
“Kweli inaonekana Humud hana nafasi Simba, viungo ni wengi na wengine ni chipukizi tena wenye uwezo mkubwa kuliko yeye.
“Inaonekana hatutamsajili ingawa kuna kipande cha watu kinaoenakana kumtaka, hivyo ndani ya saa chache tutakuwa na jibu,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Humud alirejea na kuanza mazoezi ya Simba licha ya kuelezwa kwamba anatarajia kuanza kuanza kazi katika klabu ya daraja la kwanza ya Jomo Cosmos.
Siku chache alisikika akiwakoromea waliokuwa waajili wake, Azam FC kwamba hawakuweka mambo yake wazi, nao wakatoa ushahidi wa mkataba na kueleza kila kitu wakionyesha kushangazwa na alichokuwa akikipigia kelele.
0 COMMENTS:
Post a Comment