OWINO AKIMDHIBITI SINO AUGUSTINO WA SIMBA... |
“Tayari kila kitu kimeisha na Mudde, Simba tumeamua kuvunja mkataba na hilo lilikuwa ni wazo kutoka kamati ya ufundi baada ya Mganda huyu kushindwa kuonyesha kiwango,” kilieleza chanzo.
Lakini Simba pia kesho itakuwa na ugeni wa beki Joseh Owino, Mganda mwingine ambaye ilimuacha wakati akiwa mgonjwa.
Owino anatua nchini leo kwa ajili ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili kuichezea Simba kwa mara nyingine.
Simba ilishaanza mazungumzo na Owino na wamekubaliana na sasa kinachosubiriwa ni mkataba huo ambao huenda wakaingia leo au kesho na kumtangaza rasmi kuwa mchezaji wake.
Simba ilianza kutamani kumrejesha tena beki huyo baada ya kuonyesha kiwango cha juu katika mechi yake ya kirafiki dhidi ya URA ya Uganda ambayo aliichezea na ikashinda kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, wiki iliyopita.
0 COMMENTS:
Post a Comment