Kocha Mkuu wa Simba, Abdallah Kibadeni, amesema anahitaji mechi
tano za kirafiki kabla ya Ligi Kuu Bara kuanza, baada ya kubaini makosa
mbalimbali kwenye kikosi chake.
Simba juzi Jumamosi ilicheza dhidi ya Kombaini ya Polisi, mchezo
wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kutoka
sare ya bao 1-1.
Katika mchezo huo, Simba haikuonyesha uwezo wa kutisha, hali
iliyosababisha mashabiki kutamka kuwa, Kibadeni awaachie timu yao.
Akizungumza jijini Dar, Kibadeni alisema
timu yake bado haijawa fiti na kabla ya ligi anahitaji mechi tano za kirafiki
kwa kuwa amebaini matatizo makubwa kwenye safu ya ulinzi.
Alisema anahitaji muda zaidi kukijenga kikosi chake kwa kuwa bado
hakijaonyesha kuwa imara kwa ajili ya ligi kuu.
“Timu nzuri ila kuna matatizo mbalimbali, hasa kwenye safu ya
ulinzi, nafikiri nikipata mechi tano za kirafiki kabla ya ligi, nitakuwa
nimepata kikosi bora.
“Bado naendelea kujenga kikosi kwa kushirikiana na benchi langu la
ufundi, hatutakiwi kuwa na hofu na timu yetu kwa kuwa muda uliobaki unaweza
kubadilisha kila kitu na tutakaa sawa kwenye ligi,” alisema Kibadeni.







0 COMMENTS:
Post a Comment