Kocha mpya wa Barcelona, Tata Martino
amekata mzizi wa fitna baada ya kuweka wazi kuwa angetaka kumuona Cesc Fabregas
anabaki katika kikosi chake.
Kauli hiyo ya Tata inamaliza kabisa
juhudi za Manchester United kutaka kumnasa kiungo huyo wa zamani wa Arsenal kwa
kuwa ilishafikisha hadi dau la pauni milioni 35.
Lakini kauli ya kocha huyo mpya
inasisitiza kuwa kiungo huyo mwenye miaka 26 ataendelea kubaki Cam Nou.
Kocha Mkuu wa United, David Moyes ndiye
alionekana kufanya kila linalowezekana kuhakikisha anamnsa Cesc.
0 COMMENTS:
Post a Comment