Barcelona imeitandika Santos 8-0 katika
mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wake wa nyumba wa Cam Npu.
Mechi hiyo ya kupasha misuli ya Kombe
la Joan Gamper, Barcelona ilionekana kiwembe na kuendeleza adhabu za kutisha
katika mechi zao za kirafiki.
Mshambuliaji Neymar aliyesajiliwa kwa
kitita cha pauni milioni 48.6, aliiongoza Barcelona kuiua timu yake ya zamani
lakini Lionel Messi akang’ara zaidi.
Alexis Sanchez, Pedrona Lionel Messi ndiyo
waliofunga mabao matatu ya mwanzo katika kipindi cha kwanza, halafu Messi
akatoa pasi ya mabao mawili kwa Adriano na Jean Marie Dongou, kabla ya Fabregas
aliyetokea benchi kupachika mengine mawili.
Neymar alikuwa katika wakati mgumu
baada ya shabiki mmoja kuvamia uwanja huku akitaka kumvamia na kumtandika.
Hata hivyo walinzi waliwahi lakini
shabiki huyo aliendelea kutoa lugha kali kwa Neymar na haikujulikana mara moja
tatizo lilikuwa ni nini.
0 COMMENTS:
Post a Comment