Na Saleh Ally, Freiburg, Ujerumani
Kocha wa Yanga, Ernie Brandts amemaliza
mafunzo ya wiki moja mjini Bremen.
Akizungumza mjini hapa, Brandts amesema
mafunzo hayo yamekwenda vizuri na leo atarejea nchini Tanzania kuendelea na
kazi yake kama kawaida.
“Kila kitu kimekwenda vizuri na sisi
makocha tumefanikiwa vizuri kwa kuwa ilikuwa ni lazima kufanya hivi.
“Leseni yangu ya ukocha inatambuliwa na
Uefa na ina daraja, hivyo ni lazima kushiriki kozi kama hizi kwa kipindi Fulani.
“Makocha lukuki kutoka timu za
Bundesliga walikuwa hapa na tumeshirikiana vizuri sana,” alisema.
Brandts alisema anarejea kwenda
kuendelea na maandalizi ya Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.
Anatarajia kutoa Dar leo mchana tayari
kuendelea na kazi yake ya kuwanoa mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment